11th December, 2019
  Gavana wa nairobi mike mbuvi sonko ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni kumi na tano pesa taslimu. Aidha gavana huyo amehitajika kutohitilafiana na uchunguzi wa kesi inayomkabili ya kutoweka kwa kima cha shilingi milioni 3 7 huku akiamriwa kutoendesha shughuli za kuongoza kaunti ya nairobi katika afisi zake za city hall.