Sonko kusalia ndani hadi Jumatano

KTN News Dec 09,2019


View More on KTN Leo

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko atasalia korokorokoni kwa siku 2 zaidi hadi siku ya jumatano ambapo itaamuliwa iwapo mahakama itakubali ombi la kumpa dhamana kwa mashtaka ya ufisadi yanayomkabili. Gavana Sonko pamoja na maafisa wengine wakuu katika  kaunti ya Nairobi walifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti ambapo walikanusha mashtaka hayo. Aidha maafisa wa polisi wa kukabiliana na fujo walifunga barabara mbalimbali ili kuzuia wafuasi wa gavana huyo kutatiza shughuli za kawaida. mwanahabari wetu Sirajurahman Abdullahi anatuarifu kwa kina.