Wakaazi wa Elgeyo walazimika kuhamia maeneo salama kufuatia maporomoko ya ardhi

KTN News Dec 03,2019


View More on KTN Leo

Baadhi ya wakazi wanaoishi kwenye bonde la Kerio wamelazimika kuhamia maeneo salama kufuatia mvua nyingi inayoendelea kunyesha na kusababisha maporomoko ya ardhi. Eneo ambalo limeathirika zaidi ni eneo la Turresia hasa wadi ya Soy Kusini ambako kumeshuhudiwa maporomoko ya ardhi kwenye sehemu mbali mbali.