.
2nd December, 2019
Wakazi wa mitaa ya Fedha na Nyayo iliyo eneo la Embakasi hapa Nairobi asubuhi ya leo wameandamana wakilalamikia hali duni ya barabara mitaani humo. Polisi walilazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanya wakazi hao wenye ghadhabu waliotatiza shughuli za usafiri katika barabara ya Outering, huku wakimlaumu Gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa kujitia hamnazo.