2nd December, 2019
Polisi katika eneo la Bamburi kaunti ya mombasa wamemuua kwa kumpiga risasi mtu mmoja anayedaiwa kuwa mwanachama wa moja wapo ya magenge ambayo yamekuwa yakiwahangaisha wenyeji wa mombasa. Inadaiwa walikuwa wameanza kuwashambulia kwa panga waendesha boda boda na wapita njia kabla ya tukio hilo. Washukiwa wengine walifanikiwa kutoroka japo na majeraha ya risasi kwa mujibu wa polisi.