25th November, 2019
Watu watano wa familia moja wamefariki usiku wa kuamkia leo kufuatia kusombwa na mafuriko katika eneo la Ngatatai kaunti ya Kajiado. Miili ya watano hao waliokuwa wakisafiri kutoka eneo la Namanga kuelekea Bisil ilipatikana majira ya saa kumi asubuhi alfajiri.
Akidhibitisha kisa hicho afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Daudi Loronyokwe amewasihi madereva kuwa makini wanapoendesha magari wakati huu wa msimu wa masika. Miili ya watano hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Kajiado