Gavana Sonko ajitetea, asema kwamba anaandamwa bure

KTN News Nov 25,2019


View More on KTN Leo

 Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko sasa anadai msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi katika kaunti ya  Nairobi ndio umechochea masaibu yake mikononi mwa tume ya maadili na kukabili ufisadi (EACC)

Sonko aliyezungumza katika mahojiano ya kipekee na Radio Maisha, anasema kwamba alihudumu kifungo chake katika jela ya Shimo la Tewa kabla ya mahakama ya rufaa ya juu kubatili kifungo chake.