Idadi ya wafu kutokana na mafuriko Pokot yaendelea kuongezeka

KTN News Nov 25,2019


View More on KTN Leo

Mkanganyiko wa idadi ya wafu imeendelea kushuhudiwa kuhusiana na maafa yaliyosabishwa na mafuriko katika kaunti ya Pokot magharibi huku serikali kuu na ya kaunti ikitoa idadi zinazokinzana.

Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang'i mapema leo alilazimika kukatiza safari yake kutokana na hali mbaya ya anga huku naibu rais William Ruto akipaa katika eneo lilo hilo.