Uhuru Kenyatta aangazia suala zima la BBI katika Ikulu ndogo ya Sagana

KTN News Nov 15,2019


View More on KTN Leo

Rais Uhuru Kenyatta Ameweka Wazi Matarajio Yake Kuhusu Ripoti Ya Jopo La Upatanishi Ya Bbi. Katika Kikao Na Viongozi Wa Eneo La Mlima Kenya Katika Ikulu Ndogo Ya Sagana, Rais Amesema Kuwa Japo Hajaiona Ripoti Yenyewe, Matarajio Yake Ni Kuwa Yataleta Upatanisha Pamoja Na Ugavi Sawa Wa Rasilimali Miongoni Wa Wakenya. Rais Vilevile Amedokeza Kuwa Viongozi Hao Watahusishwa Pindi Tu Ripoti Hiyo Itakapotolewa. Wakati Uo Huo, Rais Kenyatta Ametumia Fursa Hiyo Kuwaonya Viongozi Hao Dhidi Ya Kuwagawanya Wakaazi Wa Eneo Hilo Kwa Misingi Ya Kisiasa Haswa Za Urithi, Badala Ya Kuangazia Maendeleo. Haya Hapa Baadhi Ya Matamshi Ya Viongozi Waliokuwa Katika Kikao Hicho Baada Ya Kukutana Na Rais