Malala atimullwa kutoka chama cha ANC baada ya kuunga mkono chama cha ODM, Kibra

KTN News Nov 15,2019


View More on KTN Leo

Kamati Ya Masuala Ya Nidhamu Katika Chama Cha Amani National Congress, ANC,  Imempokonya Seneta Wa Kakamega Cleophas Malala Wadhifa Wake Kama Mwanachama Wa ANC Kwa Otuvu Wa Nidhamu Na Kutotii Sheria Za Chama. Mwenyekiti Wa Kamati Hiyo Yare Mohemmed Amesema Malala Alikiuka Sheria Za Chama Kwa Kumpigia Debe Mgombea Wa Kiti Cha ODM Kwenye Uchaguzi Mdogo Wa Kibra Uliokamilika Hivi Majuzi Kwa Kutumia Matamshi Yaliyomdunisha Mgombea Wa Chama Cha ANC, Eliud Owalo.  Kamati Hiyo Ya Nidhamu Imesema Itamualika Malala Mbele Yake Kwa Mahojiano Zaidi Kuona Iwapo Ana Tetesi Mbadala Za Kuzuia Chama Kumtimua Rasmi Na Hivo Kupoteza Nafasi Yake Kama Seneta