14th November, 2019
Tohara ya wanawake ni mila ambayo imekuwapo kwa miaka mingi. Ila kampeni na hamasisho kutoka kwa wadau, utunzi wa sera maalum na sheria mahsusi za kukabiliana na ukeketaji vimechangia zaidi ufanisi wa juhudi za kuidhibiti mila hiyo. Anavyoripoti Shadrack Mitty, kwenye makala maalum? Mwisho wa Nyembe? yapo matumaini ya kutokomeza kabisa mila na desturi hiyo dhalimu. Tayari yapo maeneo na vijiji katika kaunti ya Kajiado ambako tohara ya wanawake haipo kamwe. Yote yakiwa matokeo ya jamii kuelimishwa kuhusu sheria na adhabu kali kwa wahusika.