Polisi walionaswa wakimshambulia mwanafunzi wa chuo cha JKUAT wasimamishwa huku uchunguzi ukiendelea

KTN News Nov 12,2019


View More on KTN Leo

Maafisa wanne wa polisi walionaswa kwenye kanda ya video iliyosambaa mtandaoni wakimtandika mwanafunzi wa chuo kikuu cha JKUAT wamesimamishwa kazi hii leo. Wanne hao walimdhulumu Allan Omondi wakati wa maandamano ya wanafunzi wa chuo hicho wakilalamikia hali mbaya ya usalama karibu na chuo hicho.