43.3% ya vijana waKenya wanaohitimu wamekosa nafasi za ajira

KTN News Apr 01,2019


View More on KTN Leo

Ukosefu wa nafasi za ajira kwa vijana wanaohitimu katikavyuo mbalimbali ni kitendawili ambacho kinaendelea kukosa kuteguliwa. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mamlaka ya ajira nchini (National Employment Authority) Dishon Atemo, idadi hiyo sasa imefikia asilimia arobaini na tatu nukta tatu. Hii ni licha ya ufadhili wa benki ya dunia wa dollar za marekani milioni mia moja hamsini kwa mradi wa hazina ya kubuni nafasi za ajira kwa vijana. Haya yalisemwa kwenye hafla ya kufuzu kwa wanafunzi katika chuo cha Queens College huko Rongai.