27th March, 2019
Viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara kutoka Lagdera kaunti ya Garissa wanamtaka waziri wa usalama wa ndani fred matiang'i atume maafisa wengi wa usalama katika eneo hilo, kutokana na utovu wa usalama eneo hilo. watu wawili waliuawa huko Lagdera mwishoni mwa juma, ambapo sasa wanawashutumu baadhi ya viongozi kwa kuchochea hali hiyo.