16th March, 2019
Katika masuala elimu, Rais Uhuru Kenyatta hii leo amesisitiza kuwa mpito wa asilimia 100 wa wanafunzi kutoka shule ya msingi kuelekea shule ya upili. Hii ni baada ya baadhi ya washikadau kulalama kuwa shule nyingi za upili hazina uwezo wa kuwa na wanafunzi wengi kuliko kiwango. Rais alikua akizungumza katika shule ya upili ya mang`u ambapo wanafunzi waliotoa matokeo bora katika mtihani wa kitaifa walituzwa.