Mshukiwa aliyenaswa kwa makosa ya kusafiirsha dawa za kulevya amekanusha madai

KTN News Feb 23,2019


View More on KTN Leo

Mshukiwa aliyenaswa hapo jana na maafisa wa idara ya upelelezi kwa makosa ya jinai (DCI) akisafiirsha dawa za kulevya zinazoaminika kuwa aina ya heroin alizoficha ndani ya matunda kadhaa ya papai sasa amekanusha madai ya kuhusika katika biashara haramu ya dawa za kulevya. Joseph ngendo  njau alinaswa hapo jana akingia nchini kutoka nchini uganda amechapisha picha kwenye mtandao wa kijamii wa twitter akidai kuwa yeye ni mwanaharakati wa kupambana na dawa za kulevya nchini. Lakini polisi wanasema ametumia uanaharakati wake kuficha uhalifu anaofanya.