Mwanafunzi wa kidato cha tatu amekufa maji alipokuwa akiogoelea katika mto

KTN News Feb 19,2019


View More on KTN Leo

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Mutige Kaunti ya Kirinyaga amekufa maji alipokuwa akiogoelea katika mto rwamuthambi kijiji cha getuya. Kijana huyo aliandamana na wenzake jana kuogelea katika mto huo, lakini hakubahatika kutoka salama. Inaarifiwa kuwa  kijana huyo mwenye umri wa miaka kumi na saba alijaribu kuomba msaada wa wenzake lakini  kasi ya maji iliwazidi wenzake. Wenyeji walikusanyika kwenye juhudi za kuutafuta mwili wake ambao ulikuwa ungali haujapatikana.