Siku tano tangu kupotea kwa Mwanaharakati Caroline Mwathi

KTN News Feb 11,2019


View More on KTN Leo

Siku tano tangu kupotea katika njia tatanishi kwa Mwanaharakati wa Dandora wa kutetea haki za binadamu Caroline Mwathi bado hajulikani aliko. Wasiwasi umeanza kugubika uchunguzi huu huku maafisa wa usalama wakishikilia kuwa bado wanafanya uchunguzi. Caroline alikuwa mstari wa mbele kuripoti visa vya ukatili wa maafisa wa polisi pamoja na kupigania haki za mwananchi.