.
7th February, 2019
Kati ya bahari zote duniani, bahari hindi ndiyo ya tatu kwa ukubwa na inafahamika sana kutokana na fuo zake zinazopendeza. Ingawaje wengi huenda eneo la pwani kubarizi, eneo hilo ndipo jamii nyingi huita nyumbani haswa wakazi wa kaunti ya lamu na uvuvi ndio kitega uchumi chao Kikuu. Idadi ya samaki imepungua jinsi miaka inavyosonga, lakini sasa jamii zimeungana ili kuhifadhi viumbe wa baharini Kama vile samaki na pweza