Shughuli za matibabu katika Kaunti 7 nchini zimerejelea

KTN News Feb 05,2019


View More on KTN Leo

Shughuli za matibabu katika Kaunti 7 nchini zimerejelea hali yake ya kawaida baada ya wauguzi waliokuwa wanagoma kusitisha mgomo wao. Kaunti hizo ni mandera, vihiga, tharaka nithi, nyandarua, nyeri, kitui na kiambu. Wauguzi hao wameweza kusitisha mgomo baada ya serikali za kaunti hizo kukubaliana na wauguzi wao jinsi watalipwa marupurupu ya utendakazi na yale ya sare kama walivyotia saini mkataba wa maeleweno mwaka 2017. Lakini hali ni tofauti katika kaunti za Pokot magharibi, Kisumu, Nairobi, Kisii, Taita Taveta, Trans Nzoia, Elgeyo marakwet na Wajir.