Thailand inafahamika kwa mbinu za kukanda mwili almaarufu ‘Thai traditional massage’

KTN News Feb 02,2019


View More on KTN Leo

Nchi ya Thailand inafahamika sana kwa umaarufu wake wa fukwe nzuri na maeneo yaliyo na utajiri mwingi wa kihistoria. Lakini usilolijuani kuwa  nchi hiyo iliyoko kusini mashariki mwa bara la ashia pia inafahamika kwa  mbinu zake za kukanda mwili almaarufu kama thai traditional massage. Nchini Thailand, kukanda mwili hakufanyiki kwa minajili ya kutuliza tu, mbali pia ni mojawapo ya njia mbadala za matibabu. Sekta hiyo ni kiungo muhimu sana kwa uchumi wa nchi hiyo kiasi ya kuwa serikali ya thailand hudhibiti shughuli hiyo inavyoendeshwa.