.
2nd February, 2019
Wakiongozwa na Seth Panyako, Muungano wa wauguzi wa kitaifa (KNUN) umetangaza kuanza rasmi kwa mugomo wa wauguzi kuanzia siku ya jumatatu katika kaunti kumi na moja zinazojumuisha kaunti ya pokot magharibi, Nairobi, Kisumu, Taita Taveta, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet, Nyeri miongoni mwa zingine. Muungano huo ukitangaza maandamano katika kaunti tatu za Kiambu, Homabay na marsabit yataanza tarehe 6 kwa kutotekeleza makubaliano ya nyongezo ya malipo iliyohitimisha mugoma wa mwaka jana.