Rais Uhuru Kenyatta ameapa kuzidisha vita dhidi ya ugaidi

KTN News Jan 22,2019


View More on KTN Leo

Rais Uhuru Kenyatta ameapa kuzidisha vita dhidi ya ugaidi na kuwa serikali yake itapambana vilivyo na magaidi. Katika kikao na makamishna pamoja na makamanda wapya katika ikulu ya Mombasa Rais Kenyatta pia aliwaonya maafisa watakaojihusisha na ufisadi kuwa watapigwa kalamu.