Polisi wamemtia mbaroni mwanaume mmoja anayekisiwa kuhusika kwenye mauaji ya watotoe

KTN News Jan 22,2019


View More on KTN Leo

Polisi katika mtaa wa shauri moyo hapa jijini wamemtia mbaroni mwanaume mmoja anayekisiwa kuhusika kwenye mauaji yenye utata. Joseph simiyu anadaiwa kuwauwa wanawe wawili kwa kuwapa sumu jumapili usiku. Walioshuhudia wamesema kuwa aliificha miili ya bintii zake baada ya kuwau hadi mapema leo alipoamsha jirani zake na kudai kuwa alivaamiwa na wezi waliwauwa wanawe. Kulingana na majirani, simiyu na mkewe wamekuwa wakizozana kwa muda mrefu, jambo lililomfanya mkewe kurudi kwa wazazi wake wakati wa tukio. Miili ya watoto hao ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya city. Uchunguzi umeanzishwa kubaini kiini cha tukio hilo.