Polisi wakamata washukiwa wanaoaminika kupanga njama ya shambulizi ya Dusit

KTN News Jan 19,2019


View More on KTN Leo

Maafisa wa polisi wanaochunguza shambulizi la kigaidi katika mkahawa wa kifahari wa Dusit mtaa wa Riverside Drive siku ya jumanne wameendelea na operesheni ya kamatakamata dhidi ya washukiwa wanaoaminika kupanga njama ya shambulizi hilo. Mapema hivi leo polisi wamewakamata washukiwa wanne katika mkahawa wa parkside villa mjini kitui.  Watatu kati ya washukiwa hao ni raia wa kigeni na mkenya mmoja na wako njiani kuletwa hapa jijini Nairobi.