Charity Ngilu na Seneta wa Kitui Enoch Wambua walumbana hadharani

KTN News Jan 07,2019


View More on KTN Leo

Vita vya maneno vilizuka baina ya Gavana wa kaunti ya Kitui Charity Ngilu na seneta wa kaunti hiyo Enoch Wambua kuhusu usimamizi na ubadhirifu wa fedha za kaunti hiyo. 
 
Viongozi hao walilumbana hadharani walipohudhuria kutawazwa kwa askofu wa kwanza wa kanisa la AIC eneo la Mwingi, hafla iliyoongozwa na Askofu Cyrus Yego.