Mgomo wa KNUT umeshitishwa na mahakama

KTN News Jan 02,2019


View More on KTN Leo

Mahakama inayohusika na mizozo ya wafanyikazi nchini imekitaka chama cha walimu kusitisha mgomo wa walimu uliostahili kuanza hapo kesho. Jaji byram ongaya akitoa uamuzi huo kadhalika ameiagiza tsc kusitisha uhamisho wa maafisa wa knut kwa shule mbalimbali. Aidha ametaka mazungumzo ya upatanishi baina ya tsc na knut kuendelea na kzitaka pande zote kurejea mahakamani tarehe 17 mwezi huu. Wakili wa KNUT Paul Muite alitaka wanafunzi wafungue shule jumatatu ijayo jambo lililopingwa na wakili wa tsc tomin oyucho. Shule zote nchini zilitakiwa kufunguliwa hapo kesho.