.
20th December, 2018
Mtu mmoja amefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea sehemu ya ngata katika barabara ya nakuru – eldoret. Aliyefariki ni dereva wa basi lililogongana na lori. Basi hilo lilikuwa likitoka nairobi na kuelekea butere. Majeruhi wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya nakuru.