17th December, 2018
Viongozi wa kaunti ya Trans Nzoia wakiongozwa na Gavana wao Patrick Khaemba wamekashifu vikali kisa kilichotokea hapo jana katika eneo la Kolongolo ambapo inadaiwa maafisa wa polisi waliwauwa watu watano na kuwajeruhi wengine kadhaa. Akizungumza katika hospitali ya Kitale, Gavana Khaemba ameshinikiza kukamatwa kwa maafisa hao ambao anasema walikiuka sheria kwa kufyatulia raia risasi wakati wa makabiliano kati ya wenyeji na maafisa wa polisi.