.
16th December, 2018
Hatua ya wizara ya elimu hapo jana kuahirisha mtaala wa elimu ya 2 6 6 3 kwa mwaka mmoja tena imeendelea kupokea hisia mseto kutoka kwa washikadau mbali mbali huku wengi wao wakilalamikia kutohusishwa kwenye maamuzi yanayohusu elimu nchini.
Shirikisho la kutetea maslahi ya walimu wa shule za chekechea early childhood education limesema hatua hiyo imewaacha kwenye njia panda kuhusiana na hatma ya watoto wanaofaa kuanza shule mwaka ujao.