Katibu mkuu wa COTU Atwoli aonya dhidi ya kukata mishahara ya wafanyi kazi

KTN News Dec 13,2018


View More on KTN Leo

Muungano wa Kitaifa wa Walimu nchini KNUT umeikashifu serikali kwa kile walichokitaja kuwa kutowahusisha katika ubunifu wa sera na mipangilio . Katibu mkuu Wilson Sossion amekariri kwamba ni makosa kukata mishahara ya walimu kugaramia mpango wa kuwajengea wafanyikazi wa umma pasi na makubaliano. Katibu mkuu wa chama cha wafanyikazi Francis Atwoli naye ameonya dhidi ya kukata mishahara ya wafanyi kazi kabla ya kuweka mikakati ya fedha hizo jinsi zitakavyotumika. Waliyasema haya kwenye kongamano la kila mwaka la muungano wa kitaifa wa walimu katika ukumbi wa Bomas hapa jijini Nairobi.