.
8th December, 2018
Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta ya kumteua aliyekuwa Makamu wa Rais Moody Awori katika bodi ya tamaduni na vijana imeibua hisia mseto miongoni mwa viongozi wa kisiasa. Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ambaye amemtetea rais huku akisema kuwa kauli ya rais ilioonekana kuwahusisha vijana na ubadhirifu wa fedha ilinukuliwa vibaya. Mbunge huyo aliyasema haya baada ya kuzuru soko la karatina.