Wizara ya Ardhi iwaahidi waakazi wa Laikipia kuhakikisha wamepata hati za mashamba

KTN News Dec 05,2018


View More on KTN Leo

Wizara ya Ardhi imeahidi kutolegeza kamba kuhakikisha wakazi katika Kaunti ya Laikipia wamepata hati miliki za ardhi. Akizungumza mjini Nanyuki, Waziri Faridah Karoney amesema kuwa wizara yake ipo katika mikakati ya kutoa hati miliki 35,000 kwa wakazi hao. Waziri huyo aliyasema hayo aliphodhuria hafla ya kupokea malalamishi na maoni ya wakazi kuhusu ardhi. Awali, wakazi kupitia kwa waakilishi wao walilalamikia jinsi shughuli huendeshwa katika wizara hiyo. Kaunti ya Laikipia imeshuhudia visa kadhaa vya utapeli wa ardhi.