Kiongozi wa Mashtaka Hajji afafanua hatua yake ya kumteua wakili wa kutoka Uingereza

KTN News Dec 05,2018


View More on KTN Leo

 

Kiongozi wa Mashtaka ya Umma Noordin Hajji amefafanua kwa wakenya hatua yake ya kumteua wakili wa malkia wa Uingereza kuongoza kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji mkuu Philomena Mwilu. Hajji amesema kjwama wakili Khawar Qureshi atasimamia kesi hiyo kutokana na kwamba mawakili wa tajriba humu nchini hawako tayari kusimamia kesi inayohusu ubadhirifu wa mamilioni ya pesa, na ambayo inatishia kumaliza taaluma ya Jaji Mwilu, ya miaka thelathini na miwili.