28th November, 2018
Mojawapo ya mambo yaliyozua wasiwasi katika kongamano la kimataifa kuhusu uchumi wa baharini ni uchafuzi wa bahari kutokana na plastiki. Leo hii tunaangazia kaunti ya Kilifi eneo la Watamu pale ambapo jamii imebuni mbinu za kuondoa uchafu baharini na kutumia plastiki na uchafu mwingine kusaidia jamii.