×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Jopo la kudhibiti sekta ya boda boda nchini yabuniwa

21st November, 2018

Wizara ya Uchukuzi na ile ya Usalama imebuni jopo kazi la kudhibiti sekta ya bodaboda ili kuhakikisha usalama zaidi barabarani. Haya yanajiri wiki moja tu baada ya wizara hizo mbili kushirikiana kufanya msako dhidi ya magari ambazo hazijaafikia sheria za trafiki. Jopokazi hilo litakaloongozwa na Julius Mathenge linatarajiwa kutoa ripoti yake, kuhusu sekta ya bodaboda baada ya siku sitini ili kutoa mwongozo kamili, ya jinsi ya kudhibiti waendeshaji bodaboda kote nchini. Kulingana na Waziri James Macharia aliyekuwa akizungumza katika mkutano wa washikadau katika sekta ya Uchukuzi, waendeshaji bodaboda sasa wanafaa kuwa waangalifu na wenye nidhamu ya juu barabarani.

.
RELATED VIDEOS