20th November, 2018
Vijana 250 wanaohudhuria kongamano la vijana viongozi wa Afrika Mashariki linalofanyika mjini Arusha nchini Tanzania wamekosoa mwenendo wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki katika utekelezaji wa malengo 17 ya ajenda 2030 ya maendelo endelevu (sdgs) yanayohimiza serikali, asasi za kiraia na mashirikia ya kibinadamu kuchukua hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.