17th November, 2018
Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi COTU Francis Atwoli amekashifu vikali vifo na majeraha ambayo yamesababishwa na wahudumu wa boda boda kwa kukosa kutii sheria ya barabarani. Atwoli ambaye alikuwa anazungumza katika hafla ya mazishi mjini mwea kaunti ya kirinyaga, ameshinikiza waziri wa uchukuzi pamoja na yule wa usalama kutolegeza kamba katika msako unaoendelea
wa kurejesha nidhamu barabarani.