.
17th November, 2018
Mkutano wa wakulima kutoka North Rift mjini Eldoret kuhusu bei ya mahindi na malipo ya wakulima ulifanyika hii leo ambapo mbunge Alfred Keter wa nandi hills, joshua kutuny wa cherangany na silas tiren wa moiben wamependekeza gunia la mahindi la kilo tisini linunuliwe kutoka kwa wakulima kwa shilingi 3,600. Majuma machache yaliyopita serikali ilikuwa imetangaza kununua mahindi kutoka kwa wakulima kwa shilingi 2, 300 kwa gunia la kilo tisini, bei ambayo ilipingwa vikali na wakulima.