Gavana wa Nyandarua Francis Kimemia kuhojiwa kuhusu uhasama dhidi ya Spika

KTN News Nov 08,2018


View More on KTN Leo

 

Kamati ya seneti inayoshughulika na masuala ya ugatuzi imemtaka Gavana wa Nyandarua Francis Kimemia kufika mbele ya kamati hiyo wiki ijayo.  Hii inafuatia madai kwamba Gavana Kimemia anachochea uhasama kati ya mawaziri wa serikali ya kaunti hiyo na wawakilishi wa wodi ili kumfurusha spika wa kaunti hiyo. Tayari, ukumbi unaojumuisha maspika wa serikali za magatuzi wamefikisha hoja kwa seneti wakitaka kulindwa dhidi ya njama za kuwafurusha wanaposukumiza uwajibikaji katika matumizi ya pesa ya umma.