24th October, 2018
Hatimaye gavana wa kaunti ya Migori Zachary Okoth Obado ameachiliwa huru kwa thamana katika kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno ambaye pia alikuwa mpenzi wake. Obado ameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni tano pesa taslimu na uthamini wa kiasi sawa na hicho mara dufu.