22nd October, 2018
Mbunge wa Manyatta John Muchiri amependekeza mageuzi ya katiba kupunguza mishahara ya viongozi waliochaguliwa. Muchiri anataka viongozi hao kupata laki moja tu kila mwezi, bima ya afya na pesa za mafuta ya gari. Hata hivyo anataka madaktari, wauguzi, maafisa wa usalama na wengine wanaotangamana na umma moja kwa moja kupata mishahara ya juu ili kurahisha utoaji wa huduma. Aidha ametoa wito kwamba jukumu la kugeuza katiba lisiachiwe wanasiasa tu.