.
22nd October, 2018
Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua ameanzisha mchakato wa kudhibiti idadi ya raia wa kigeni wanaofanya biashara au kazi ambazo wakenya wana uwezo wa kuzifanya humu nchini. Gachagua ametangaza kuwa atawasilisha mswada bungeni kupiga marufuku raia wa kigeni kupewa zabuni inayozidi shilingi bilioni moja na zabuni hizo kutengewa makampuni yanayomilikiwa na wakenya. Amesema kampuni za wachina zimewanyima wakenya fursa ya kibiashara.