.
14th October, 2018
Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini Francis Atwoli, amesema kwamba mabadiliko ya katiba ili kuimarisha uwakilishwaji serikalini kutaimarisha amani na imani ya waekezaji nchini. Wakizungumza katika sehemu ya Kyumbi kaunti ya Machakos kwenye zoezi la kuchangisha pesa za ujenzi wa kanisa, Atwoli amewakaripia wanaopinga mabadiliko hayo na kusema kwamba wana ubinafsi. Wakiwa pamoja na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa na seneta wa kakamega Cleophus Malala, wote waliunga mkono mabadiliko ya katiba kwa manufaa ya wakenya wote.