.
13th October, 2018
Ni matumaini ya kila mzazi anapojaliwa na mtoto kuwa mwanawe ataishi maisha marefu yasiyo na bugdha. Lakini taswira hii ni tofauti kwa watoto wenye ugonjwa wa kulegea misuli yaani duchenne muscular dystrophy. Ugonjwa huu ambao huwapata watoto wa kiume tu hauna tiba na huathiri na kuilemaza misuli muhimu mwilini na wengi wao hawaishi kupita umri wa kubaleghe.