Wamiliki wa basi lilohusika kwenye ajali katika eneo la Fort Tennan Kericho wafikishwa mahakama

KTN News Oct 11,2018


View More on KTN Leo

Wamiliki wa basi lilohusika kwenye ajali mbaya ya barabara katika eneo la Fort Tennan Kericho, walifikishwa mahakama ya Molo alhamisi asubuhi.

Bernard Shitiabayi na Cleophas Shimanyu walikamatwa katika kaunti ya Kakamega jumatano na kufikishwa mbele ya hakimu Samuel Wahome. Japo polisi waliomba muda zaidi wa kufanya upelelezi hakimu alisema kuwa atatoa kauli yake ijumaa.