KNUT sasa kimetoa muda wa siku kumi na nne kwa tume ya kuwaajiri walimu

KTN News Oct 04,2018


View More on KTN Leo

Na katika hatua ambayo huenda ikavurugu maandalizi ya mitihani ya kitaifa chama cha kutetea maslahi ya walimu, KNUT, sasa kimetoa muda wa siku kumi na nne kwa tume ya kuwaajiri walimu, TSC, kutimiza ahadi ilizotoa kwa waalimu lau sivyo walimu watafanya mgomo. 

Katibu mkuu wa KNUT, Wilson Sossion, amewashutumu viongozi wa  TSC kutokana na kile anachokitaja kuwa kukosa kuwajibika na kusababisha mahangaiko kwa walimu kila mwaka.