26th September, 2018
Siku chache baada ya naibu wa Rais William Ruto kudai kuwa ongezeko la gharama ya maisha halijasababishwa na sheria mpya ya ushuru wa ziada kwa bidhaa za petroli bali ni wafanyibiashara walaghai, sasa inaelekea wenyeji wa eneo la Kapsoya mjini Eldoret wanakubaliana naye ambapo wamewagomea wahudumu wa matatu ambao wamewashutumu kwa kuongeza nauli kiholela kwa kisingizio cha kupanda kwa ushuru wa vat.Abiria hao waliamua kutembea kwa miguu na wengine kutumia pikipiki kama njia mojawapo ya kueleza ghadhabu yao dhidi ya wahudumu wa matatu. Halikadhalika walizitaka idara zinazohusika kuwajibika na kuainisha nauli katika sekta ya matatu