.
26th September, 2018
Ghadhabu za wakulima wa mahindi zimeshuhudiwa leo katika kikao cha seneti mjini Eldoret kuhusu zogo la kucheleweshwa kwa malipo yao licha ya kuwasilisha mahindi katika maghala ya halmashauri ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB. Wakulima walitumia fursa hiyo kuwapasha maseneta katika kikao hicho maalum. Hata hivyo seneta wa Baringo Gideon Moi aliwasilisha muswada wake ambao ungeleta mabadiliko ya kudumu kwa halmshauri ya nafaka na mazao nchini ili kutatua matatizo yanayowakabili wakulima