.
25th September, 2018
Polisi wamedhibitisha kumkamata mshukiwa mmoja katika mauaji ya Monica Kimani katika mtaa wa Kilimani jumatano iliyopita. Mshukiwa huyo ambaye ametajwa kwa jina la Joseph Kuria Irungu alikamatwa saa kumi na moja alfajiri ya leo akiwa nyumbani kwake katika mtaa wa langata hapa jijini Nairobi.